Pata maelezo ya wakati halisi kuhusu mahali magari yako yapo kwa muda uliobainishwa awali. Kando na hii unaweza kupata taarifa za ziada kuhusiana na chombo chako.
Maelezo yanayohusiana na safari yanapatikana kupitia kifaa cha kufuatilia kilichofungwa kwenye gari. Data hii inasaidia katika kuchanganua vigezo mbalimbali kama vile kasi, kusimama, jumla ya umbali uliosafiri.
Pata taarifa kupitia SMS na barua pepe wakati wowote magari/madereva wanapofanya shughuli ambazo hazijaidhinishwa. Bainisha kiwango cha juu cha kasi, muda wa kusimama, n.k, na taarifa za kutofuata kanuni zitatolewa.
PowerTrack hutoa Ufuatiliaji na Uchambuzi wa Magari kwa Wavuti kama "Huduma". Huduma hii hukuruhusu kufuatilia kwa kina mali yako kupitia simu kwa eneo, kasi ya kupita kiasi, kusimamishwa bila ruhusa, na hukupa taarifa pamoja na ripoti za kina. Huduma hiyo inapatikana kwa kuingia kwenye tovuti yetu na pia kwa kupiga simu kituo chetu cha usaidizi.
Inatumia teknolojia ya GPRS kukuambia mahali gari lako lilipo kila wakati. Kutakuwa na vifaa viwili vilivyofungwa kwenye gari lako. Moja ni processor, na moja ni antenna. Antenna itatoa ishara na kuruhusu processor kujua ni wapi.
Processor itafanya taarifa ipatikane kwenye mtandao na kwenye simu yako ya mkononi. Pia ina vitambuzi vinavyoweza kukujulisha Muda ambao gari lako lilisimamishwa, na iwapo injini ilikuwa imewashwa au kuzimwa wakati huu ili kuzuia upotevu wa mafuta. Itakuambia ikiwa mikanda ya kiti imefungwa na ikiwa milango ya cabin imefunguliwa au imefungwa. Na habari nyingi zaidi!
Ni kama kwamba umeketi na kufuatilia kila moja ya gari lako wakati wote.
Zingatia upanuzi wa biashara yako - Kwa maelezo zaidi & onyesho, Wasiliana Nasi!
Tembelea Tovuti yetu: http://powertrack.co.tz/