Tunajitahidi kuongoza tasnia ya Tehama nchini Tanzania katika kuleta teknolojia ya kisasa na ya hali ya juu zaidi, pamoja na suluhu tofauti kwa mahitaji yote yanayowezekana ya wateja wetu.
Tulianza mwaka 2001, tukiwa na wafanyakazi 4; leo, sisi ni vinara katika fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na Uendeshaji wa Ofisi nchini Tanzania.
Tumekua kwa kiasi kikubwa na kuwa na matawi kwenye miji zaidi ya 16 nchini Tanzania na wateja kote Afrika Mashariki. Kwa wafanyakazi wa moja kwa moja zaidi ya 100 na idara kuu 9, tunafanya kazi na wateja katika kila sekta na kutoka kwa biashara ndogo za kati hadi biashara kubwa na mashirika ya serikali.
Tunajishughulisha na aina mbalimbali za bidhaa na huduma ili ukija Power Computers, sio tu tukuuzie bidhaa, lakini upate SULUHISHO kamili ili biashara yako uiendeshe vizuri iwezekanavyo. Usichelewe. Songa mbele kuelekea kwenye mafanikio. Tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu uchukue hatua yako ya kwanza katika ulimwengu wa chaguo bora zaidi.